Home Uncategorized KOCHA WA YANGA KUTUA LEO BONGO

KOCHA WA YANGA KUTUA LEO BONGO


 KOCHA Cedric Kaze anayekuja kushika mikoba ya kuifundisha Yanga, yupo safarini kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuanza rasmi majukumu yake mapya.

Ofisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli, amethibitisha ujio wa Kocha huyo ambaye mapema leo alikuwa jijini Amsterdam Uholanzi, kwaajili ya kubadilisha ndege ya kumleta Tanzania.

Kaze anatarajiwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa nne usiku leo kwa ndege ya Shirika la Ndege la KLM.


Anakuja kubeba mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye alifungashiwa virago Oktoba 3 baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Coastal Union.

Wakati anaondoka aliacha timu ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 13 kisha ilishushwa na Azam FC baada ya kushinda dhidi ya Kagera Sugar na Simba iliposhinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania ikashushwa mpaka nafasi ya tatu.
SOMA NA HII  ALIYETAJWA KUTUA YANGA MAMBO YAGEUKA, WASHINDWANA ' PESA NDOGO'