Home Uncategorized EYMAEL AWAWEKA CHINI YA ULINZI MASTAA YANGA

EYMAEL AWAWEKA CHINI YA ULINZI MASTAA YANGA

YANGA kumbe haitaki mchezo kwa wachezaji wake kwani, imebainika kuwa licha ya Kocha Luc Eymael kuwapa programu ya mazoezi, lakini pia amewaweka watu wa kuwafutilia nyota wake hao ili kuona kila kitu kinakwenda sawa kipindi hiki cha kupisha janga la virusi vya corona.

Kumbe unapoona mastaa wa Yanga wakijifua gym na ufukweni ili kujiweka fiti kuna watu wanawafuatilia kuhakikisha wanatekeleza kwa ufanisi programu za kocha wao aliyepo Ubelgiji kwa sasa.

Meneja wa Yanga, Abeid Mziba ‘Tekero’ aliliambia Mwanaspoti kwa wachezaji hao haikuishia kocha kuwapatia programu tu bali wanafuatiliwa kujua maendeleo yao.

Alisema yeye ndiye anayefanya zoezi la kwenda kwa mchezaji mmoja mmoja kuona jinsi wanavyofanya mazoezi huku akiwapa na ushauri wa kuwa bora zaidi.

“Namfuatilia mchezaji mmoja baada ya mwingine katika mazoezi yao, wana morali ya kutosha na mazoezi yanaridhisha hivyo kocha hatakuwa na kazi ngumu,” alisema straika huyo wa zamani wa RTC, Yanga na Taifa Stars aliyekuwa mkali kwa mabao ya kichwa.

“Nimecheza najua soka ni nini, hivyo hainipi shida kuwasaidia pale ninapoona panahitajika msaada,” alisema na kuongeza kila anapozungumza na wachezaji hao anabaini wana hamu ya kufanya kazi kwa bidii huku wakisubiri ligi ianze baada ya serikali kusimamisha kwa siku 30.

SOMA NA HII  AZAM FC YACHEKELEA UWANJA WAO KUTUMIKA KWENYE MECHI ZA LIGI NA KOMBE LA SHIRIKISHO