Home Uncategorized GUARDIOLA ANAWEZA KUSEPA NDANI YA MANCHESTER CITY, SABABU YATAJWA

GUARDIOLA ANAWEZA KUSEPA NDANI YA MANCHESTER CITY, SABABU YATAJWA


EMANUEL Petit, mkongwe wa zamani wa timu ya Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa amesema kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Pep Guardiola anaweza kusepa ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo amesema sababu itakayomfanya Guardiola kusepa ndani ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England ni kushindwa kujinasua kwenye sakata la kufungiwa na UEFA..

City imefungiwa na UEFA kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa muda wa miaka miwili mfululizo kwa kuvunja sheria ya usajili na ilipigwa faini pia.

“Nafikiri Guardiola anaweza kuondoka ndani ya City kama wasipojinasua katika hili japo uamuzi unabaki kwake kwa sasa.Kwa sasa amesema kuwa amechoka kuwa kocha huenda ikawa ni sababu yake kuondoka.

“Sijui ambacho kitatokea ila hofu yangu siyo kwamba watakosa kocha mpya hapana najua atakuja kocha mwingine kwani hawezi kufundisha milele ila wasiwasi wangu ni kwenye uwekezaji wao, huenda watapa hasara,” amesema.

SOMA NA HII  LIVE:YANGA 0-0 NAMUNGO FC