Home Uncategorized HIMID MABO: BADO NINAPIGA MAZOEZI NDANI, KIKUBWA DUA TUWE SALAMA

HIMID MABO: BADO NINAPIGA MAZOEZI NDANI, KIKUBWA DUA TUWE SALAMA

HIMID Mao, nyota anayekipiga Klabu ya ENPPI ya Misri inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo amesema kuwa licha ya kuwepo kwa Virusi vya Corona bado anaendelea kufuata kanuni za afya na kufanya mazoezi akiwa ndani ili kulinda kipaji chake.

Kwa sasa ligi nyingi duniani zimesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimekuwa janga la dunia.

Akizungumza na Saleh Jembe, Himid amesema kuwa anaendelea kufanya mazoezi ili kulinda kipaji chake na kuchukua tahadhari ya Corona.

“Ninamshukuru Mungu nipo salama na ninaendelea kulinda kipaji changu kwa kufanya mazoezi licha ya kwamba ni ndani ya nyumba, kikubwa ni kuomba dua hali iwe shwari,” amesema.

SOMA NA HII  NDANDA KUMEKUCHA, JUNI SITA KUKIWASHA NA NAMUNGO