Home Uncategorized KIUNGO HUYU WA SIMBA PANGA LINAMHUSU MAZIMA

KIUNGO HUYU WA SIMBA PANGA LINAMHUSU MAZIMA


SAID Ndemla, nyota wa Simba yupo kwenye hatihati ya kuachwa na mabosi wake hao kutokana na kushindwa kufurukuta ndani ya klabu hiyo kwa sasa.

Ndemla amekuwa kwenye wakati mgumu msimu huu ambapo Simba ikiwa imecheza mechi 28 amecheza mechi tatu za Ligi Kuu Bara.

Simba ikiwa imetumia dakika 2,520 ametumia dakika 270 kuonyesha makeke yake.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa Simba ipo kwenye mpango wa kuachana na nyota huyo ambapo klabu inayotajwa kumchukua ni JKT Tanzania.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Maziginza amesema kuwa suala la kuwaacha wachezaji kwa sasa bado haliwezwi kuwekwa wazi mpaka pale ligi itakapokamilika. 

SOMA NA HII  STARS YAPEWA RAI YA KUCHUKUA KIKOMBE MISRI, LAZIMA IFUATWE