Home Uncategorized KOCHA KAGERA SUGAR AWATAKA WACHEZAJI WASIPUUZIE MAZOEZI

KOCHA KAGERA SUGAR AWATAKA WACHEZAJI WASIPUUZIE MAZOEZI



UONGOZI wa Kagera Sugar, umesema kuwa ni muhimu kwa kila mchezaji kufanya mazoezi binafsi pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona katika kipindi hiki kigumu.


Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kila mchezaji ni wajibu wake kutimiza kikamilifu majukumu yake akiwa nyumbani bila kusahau kuchukua tahadhari.

“Muhimu kwa kila mchezaji kuchukua tahadhari akiwa nyumbani dhidi ya Virusi vya Corona pamoja na kufanya mazoezi bila kuchoka.

“Kazi kubwa ya mchezaji ni kulinda kipaji chake hivyo iwapo hatafanya mazoezi ni ngumu kwake kuwa bora, ” amesema.
SOMA NA HII  SABABU ZA UWANJA WA AZAM COMPLEX KUWA SAWA NA TP MAZEMBE HIZI HAPA