Home Uncategorized MCHEKA NA NYAVU ANAYEWINDWA NA YANGA ATAJA KINACHOIMALIZA TIMU YAKE YA ZAMANI

MCHEKA NA NYAVU ANAYEWINDWA NA YANGA ATAJA KINACHOIMALIZA TIMU YAKE YA ZAMANI


MTUPIA mabao namba moja ndani ya Namungo ambaye aliwahi kucheza pia ndani ya Yanga amesema kuwa kilichokuwa kinaiponza Yanga kushindwa kutupia mabao mengi ni upepo ila uwezo wa wachezaji ni mkubwa.

Yanga ikiwa imecheza mechi 27 imefunga mabao 31 huku kinara wao wa utupiaji akiwa ni David Molinga mwenye mabao nane na mechi ambayo kwa msimu huu wa 2019/20 walifunga mabao mengi ilikuwa mbele ya Singida United ambapo walishinda mabao 3-1.

Akizungumza na Saleh Jembe, nahodha wa Namungo, Reliants Lusajo amesema kuwa kikubwa ambacho kilikuwa kinaimaliza Yanga ni upepo kuwa mbaya kwao kwa nyakati walizokuwa wakicheza.

“Ukitazama kikosi kilipokuwa kikipambana na kucheza kilikuwa kinafanya vizuri ila kikubwa kilichokuwa kinawashinda ni upepo kwa wakati kuwakataa.

“Unajua mchezo wa mpira una mabadiliko siku nyingine unaweza kukukataa na wakati mwingine ikawa fresh, bado nina amini inaweza kuwa bora kwenye upande wa kufunga mabao zaidi ya vile ambavyo mashabiki wanafikiria,” amesema.

Lusajo ametupia mabao 11 akiwa ni kinara ndani ya Namungo pia ametoa pasi tatu za mabao amekuwa akihusishwa kurejea Yanga msimu ujao.

SOMA NA HII  STARS YABEBA MATUMAINI YA KUFANYA VIZURI KESHO DHIDI YA TUNISIA