Home Uncategorized MWILI JUMBA WA YANGA ATAJA KINACHOMFELISHA

MWILI JUMBA WA YANGA ATAJA KINACHOMFELISHA


MSHAMBULIAJI wa Yanga mwili jumba, Yikpe Gnamien amesema kuwa kilichompoza ashindwe kuonesha makeke yake hivi karibuni ni kukalishwa benchi kwa muda mrefu.

Ingizo hilo jipya ambalo lilivunja mkataba na Klabu ya Gormahia limetupia bao moja kwenye ligi ilikuwa ni kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Singida United.

Yikpe amesema:” kikubwa ambacho kilikuwa kinanifanya nisiwe kwenye ubora wangu ni kukaa benchi kwa muda mrefu jambo ambalo lilinifanya nishindwe kuonyesha kile nilichonacho.

“Kwa kipindi cha sasa ninachukua mazoezi binafsi ili kuwa bora nina amini nitafanya vema pale nikipewa nafasi kikubwa kwa sasa kila mmoja kuchukua tahadhari,” .

Janga la Corona limesimisha ligi ya Bongo tangu Machi 17 na mpaka sasa bado haijajulikana itarejea lini.

SOMA NA HII  LIVERPOOL YAJIPANGA KUMREJESHA NYOTA WAO WA ZAMANI STERLING WA CITY