Home Uncategorized HATMA YA MLINDA MLANGO NAMBA MOJA WA AZAM FC MIKONONI MWA MROMANIA

HATMA YA MLINDA MLANGO NAMBA MOJA WA AZAM FC MIKONONI MWA MROMANIA


RAZACK Abarola, mlinda mlango namba moja wa Klabu ya Azam FC hatma ya kubaki ndani ya Klabu ya hiyo ipo mikononi mwa Kocha Mkuu, Arstica Cioaba ambaye ni raia wa Romania.
Nyota huyo raia  Ghana amekuwa kwenye ubora wake ndani ya viunga vya Azam FC iliyo nafasi ya pili kwenye ligi na pointi zake 54 baada ya kucheza mechi 28.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi alisema kuwa masuala ya mikataba kwa wachezaji ambao bado hawajaongezewa kwa sasa inasubiri ripoti ya kocha.
“Kwa wachezaji wetu ambao mikataba yao inakaribia kumalizika msimu huu ikiwa ni pamoja na mshambuliaji Donald Ngoma, Abarola hawa wote inasubiriwa ripoti ya mwalimu ndiyo tutatoa taarifa kuhusu kuwaongezea mikataba,” alisema Zakazi.
SOMA NA HII  MATOKEO YA MECHI ZA LEO JUNI 27 VPL