Home Uncategorized WAMEJIPANGA…KWA SIMBA HII MNACHEZA NYIE..!!

WAMEJIPANGA…KWA SIMBA HII MNACHEZA NYIE..!!

HAIELEWEKI Ligi Kuu msimu huu itaendelea lini, lakini straika Mnigeria Raphael Obinna amesema hakuna miujiza yoyote inayoweza kutokea Simba ikakosa ubingwa.

Mchezaji huyo tegemeo wa Mwadui FC ya Shinyanga ameenda mbali zaidi na kusema kwamba kwa uzoefu wake na jinsi alivyoona ubora wa timu zote hata msimu ukianza upya leo Simba itabeba tu kombe hilo kwani haina mpinzani.

Ligi hiyo imesimama kutokana na janga la corona, lakini Simba kitakwimu inapewa nafasi kubwa ya kutetea ubingwa huo kutokana na ufanisi na kasi yake.

Obina mwenye mabao sita katika Ligi Kuu msimu huu, alisema kwa sasa Simba wanaonekana kuwa bora zaidi kuliko watani zao wa jadi, Yanga na hata Azam FC kuanzia mchezaji mmojammoja pamoja na mambo ya ndani ya nje ya uwanja.

Anasema kwamba kitendo cha Simba kuingiza mguu kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kiliwapa mzuka na kuongeza zaidi ubora wao uwanjani pamoja na mipango yao, kwani inaonekana hesabu zao ni kurejea tena anga hizo kwa namna yoyote ile.

“Yanga na Simba wana timu nzuri zenye uwezo mkubwa kiushindani, nimeiona hata Azam, ambacho Simba wamewazidi wapinzani wao ni kwamba wana mwendelezo wa kupata matokeo mazuri tofauti na wengine.

“Wanaweza kuchukua ubingwa hata kama msimu ukifutwa na kuanza tena, wanaweza kuendelea kufanya vizuri, wana kila kitu cha timu bora ya ushindani. Natoa kwao asilimia kubwa,” alisema nyota huyo wa Mwadui ambayo lengo lake ni kusalia kwenye ligi tu msimu huu ili wajipange upya.

Obina alisema mbali na kufutwa kwa msimu hatua ambayo inaweza kufikiwa kama hali haitakuwa shwari, alitoa ushari kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa waige kile ambacho Shirikisho la Soka Italia wameafikiana.

Inaelezwa kuwa pindi ambapo hali itakapokuwa shwari Italia, basi Ligi Kuu nchini humo ambayo ni maarufu kama Serie A itachezwa milango ikiwa imefungwa yaani bila mashabiki kuingia viwanjani.

“Hiyo inaweza kuwa namna nzuri ya kumaliza ligi kama itaonekana kufutwa kwa msimu ni jambo gumu,” alisema mchezaji huyo ambaye miaka miwili iliyopita alicheza Ligi Kuu Zanzibar ambayo klabu nyingi zimekuwa zikilia ukata.

SOMA NA HII  BREAKING; SIMBA YASAJILI WABRAZIL WATATU

Simba ndio wanaoongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 71, Azam wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 54, Yanga inashika nafasi ya tatu pointi 51 huku Namungo wakiwa na pointi 50 katika nafasi nne.

Rais wa TFF, Walace Karia amekuwa akisisitiza kwamba kila kitu kitasimama kama kawaida mpaka watakapopata muongozo wa Serikali.

Karia amekiri kusikia maoni kutoka kwa wadau kuhusiana na kufuta msimu au kucheza bila mashabiki, lakini hawawezi kuchukua hatua yoyote kwa sasa kwa madai kwamba ni mapema.

Gwambina ambayo ina nafasi kubwa ya kupanda Ligi Kuu imetaka ligi imalizikie uwanjani kwa madai kwamba wanaong’ang’ania msimu ufutwe hali zao ni tete uwanjani.