Home Uncategorized ALIYEZICHONGANISHA SIMBA NA YANGA ANUKIA KUTIMKIA MOROCCO

ALIYEZICHONGANISHA SIMBA NA YANGA ANUKIA KUTIMKIA MOROCCO

KIUNGO wa Polisi Tanzania, anayewindwa na Simba, Yanga na Azam FC huenda akasepa zake na kuibukia Morocco kukipiga soka la kulipwa.

Baraka Majogoro ambaye msimu huu amekuwa kwenye ubora wake inaelezwa kuwa amekuwa akizichonganisha Simba na Yanga ambazo zote zinahaha kuipata saini yake.

Habari zinaeleza kuwa kuna timu moja ambayo ipo Morocco imeshaingia kwenye 18 ikisaka saini yake.

“Tayari Majogoro ameanza mazungumzo na Klabu ya Youssofia Berrechid ya huko Morocco hivyo mambo yakijibu anaweza kusepa,” ilieleza taarifa hiyo.

Majogoro amesema kuwa anatazama nafasi yake ya kucheza kwanza kisha dili lenyewe litasema nini.

SOMA NA HII  JOH MAKINI AWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA