Home Uncategorized BIGIRIMANA MTUPIAJI ANAYEZICHANYA SIMBA NA YANGA ANAPIGA KUTWA MARA TATU

BIGIRIMANA MTUPIAJI ANAYEZICHANYA SIMBA NA YANGA ANAPIGA KUTWA MARA TATU

BIGIRIMANA Blaise, raia wa Rwanda amesema kuwa kwa sasa anafanya mazoezi binafsi kutwa mara tatu ili kulinda kipaji chake.
Blaise ambaye inaelezwa kuwa ameziingiza vitani klabu kongwe Bongo ambazo ni Simba na Yanga ambazo zinahaha kupata saini yake amekuwa kwenye ubora wake msimu huu akiwa ndani ya Namungo kwa kucheka na nyavu.
Blaise amesema:-“Ninafanya kazi kwa bidii ndio maana kunakuwa na timu nyingi zinahitaji kupata saini yangu, wakati wa mapumziko ninafanya mazoezi kutwa mara tatu ili kulinda kipaji changu.
“Asubuhi nikiamka ninafanya mazoezi pia mchana kidogo ili nisijichoshe pamoja na jioni nina amini kwa kasi ambayo ninakwenda nayo nitazidi kuwa imara,” amesema.
Blaise ndani ya Ligi Kuu Bara ametupia mabao 10 kati ya 34 yaliyofungwa na timu yake iliyo nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi 50.
SOMA NA HII  TETEMO LA ARDHI LAIVAMIA KATAVI