Home Uncategorized BOXER, NYOTA YANGA AFICHUA MAANA YA JINA LAKE

BOXER, NYOTA YANGA AFICHUA MAANA YA JINA LAKE


PAUL Godfrey maarufu kama Boxer beki wa Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kupewa jina hilo ni spidi yake ya kukimbiza upepo ndani ya uwanja.
Boxer alifanya vema msimu wa 2018/19 chini ya Kocha Mkuu winyi Zahera na alimuweka benchi mkongwe Juma Abdul ambaye kwa sasa amerejea kwenye ubora wake.
Akizungumza na Saleh Jembe, Boxer amesema kuwa awali wengi walikuwa wanamuita Paul ila kutokana na spidi yake ndani ya uwanja ikabadili upepo wa jina lake.
“Nilikuwa ninaitwa Paul na wenzagu ila kutokana na spidi yangu ya kukimbia ndani ya uwanja ilinifanya nibadilishwe jina na kuitwa Boxer ambalo ni jina la pikipiki.
“Boxer inaaminika kuwa na spidi kubwa ndani ya uwanja sasa hapo wachezaji wenzagu wakawa wananifananisha na bodaboda hiyo,” amesema.
SOMA NA HII  AMRI SAID WA MBEYA CITY AFUTWA KAZI