Home Uncategorized DILUNGA AWEKA BAYANA NAMNA DILI LAKE LA KUIBUKIA YANGA LILIVYO

DILUNGA AWEKA BAYANA NAMNA DILI LAKE LA KUIBUKIA YANGA LILIVYO


HASSAN Dilunga, kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa alikuwa tayari kurejea ndani ya Yanga ila mipango imebadilika kwa sasa.

Ilikuwa inaelezwa kuwa kiungo huyo aliwekwa kwenye rada za Yanga ambao walikuwa mabosi wake wa zamani kabla ya kuachana naye akaibukia Mtibwa Sugar timu iliyomlea na sasa amerejea Simba.

Dilunga amesema:” Ndoto za wachezaji wengi wa Bongo ni kucheza ndani ya Simba ama Yanga ila zote nimetimiza kwa kuwa nimecheza timu zote kubwa. 


“Taarifa za Yanga kunihitaji nilipata nilikuwa tayari kurejea kwenye klabu yangu ya zamani ila kwa sasa sipo kwenye wakati mzuri wa kurejea huko ninataka kucheza nje ya nchi.” 

Dilunga ametupia mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara kati ya 63 yaliyofungwa na Simba yenye pointi 71 ikiwa nafasi ya Kwanza.

SOMA NA HII  YANGA WAIPA SAPOTI SIMBA KIMATAIFA, WAPANIA KUWAKALISHA ROLLERS LEO TAIFA