Home Uncategorized HAMIS KIIZA ATOA SOMO HILI KWA WACHEZAJI WATAKAOPATA MADILI MAPYA

HAMIS KIIZA ATOA SOMO HILI KWA WACHEZAJI WATAKAOPATA MADILI MAPYA


HAMIS Kiiza, mshambuliaji wa zamani wa Yanga
na Simba amewataka wachezaji watakaopata nafasi ya kuzitumikia timu mpya msimu ujao lazima watambue thamani yao pamoja na timu kiujumla.

Kiiza akiwa Bongo alicheza jumla ya mechi 110 za ligi ambapo alitupia mabao 80, 56 alifunga akiwa Yanga na 24 alitupia akiwa Simba.

 “Muhimu kwa mchezaji atakayepata nafasi ya kucheza kwenye timu mpya akatambua thamani yake kwanza kisha ile ya timu ndipo itakuwa rahisi kwake kufanikiwa. 

“Akishatambua thamani yake maana yake atakuwa na nidhamu nje na ndani ya uwanja, atapambana kufikia mafanikio huku akiheshimu jezi ya timu ambayo imempa kandarasi ya kuitumikia timu hiyo,” amesema.

 Kwa sasa Kiiza anakipiga ndani ya Klabu ya Proline FC iliyopo nchini Uganda.

SOMA NA HII  NIYONZIMA: AFYA NI MUHIMU, TUCHUKUE TAHADHARI