Home Uncategorized HASIRA ZA LUKAKU BADO ZINAWAKA KWA KOCHA WAKE

HASIRA ZA LUKAKU BADO ZINAWAKA KWA KOCHA WAKE

Verified

ROMELU Lukaku, mshambuliaji wa Klabu ya Inter Milan ya Italia amesema kuwa hawezi kumsamehe kocha wake wa zamani wa Chelsea Andre Villas Boas.

Sababu kubwa anasema kuwa  alimuacha katika kikosi cha UEFA Champions League 2011/12 cha Chelsea kilichotwa Ubingwa.

“Hili taji (UCL) ni moja kati ya mataji niliyokuwa nayaota, unatakiwa usherehekee ubingwa ule ukiwa kwenye timu lakini kuna mtu mmoja ambaye alinitoa (Kikosini) kocha aliyepita (Andre Villas-Boas) sitamsamehe kamwe, katika sherehe zile sikushika lile Kombe (UCL) kwa vidole vyangu sababu sikuwa nimeshiriki kulitwaa,” amesema.

Lukaku aliibukia Chelsea 2011 kwa uhamisho wa paundi milioni 17 lakini hakupata nafasi chini ya kocha Andre Villas-Boas na hakumjumuisha katika kikosi cha Champions League 2011/2012.

SOMA NA HII  BEKI WA MANCHESTER UNITED ASHINIKIZA KUSEPA MAZIMA