Home Uncategorized MESSI:CORONA IMETIBUA SHANGWE YA KUTWAA UBINGWA

MESSI:CORONA IMETIBUA SHANGWE YA KUTWAA UBINGWA


RAMADHAN Singano, ‘Messi’ nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya TP Mazembe amesema  kuwa janga la Corona limetibua shangwe za ubingwa ambao wameutwaa hivi karibuni.

Mazembe ilitangazwa kubeba ubingwa na Shirikisho la Soka nchini humo kutokana na janga la Virusi vya Corona kuivuruga vuruga dunia.

Akizungumza na Saleh Jembe, Messi amesema kuwa wamefurahi kutwaa ubingwa ila hakukuwa na shangwe kubwa kutokana na Corona.

“Tumefurahi kutwaa ubingwa ila hakukuwa na shangwe kutokana na janga la Virusi vya Corona kwani hakuna mikusanyiko inayoruhusiwa,” amesema.

Messi yupo pamoja na rafiki zake wawili ambao ni Eliud Ambokile na Thomas Ulimwengu wakiipeperusha bendera ya Tanzania nchini Congo.

SOMA NA HII  SIMBA, WALTER BWALYA MAMBO SAFI