Home Uncategorized MITAMBO HII NANE YA KAZI YAINGIA ANGA ZA YANGA

MITAMBO HII NANE YA KAZI YAINGIA ANGA ZA YANGA


INAELEZWA kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye hesabu za kuboresha kikosi chake msimu ujao ili kuleta ushindani kwenye mechi za ligi na mashindano mengine.

Tayari kwa sasa kuna majina ambayo yanatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi hao wa Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu Luc Eymael.

Wazawa wanaotajwa kuwa kwenye rada za Yanga kwa sasa hawa hapa:-Relliats Lusajo wa Namungo, Bigirimana Blaise wa Namungo hawa ni washambuliaji huku kiungo Luka Kikoti naye akiwa kwenye orodha.

Bakari Mwamnyeto na pacha wake Ibrahim Ame mabeki wa Coastal Union, Baraka Majogoro wa Polisi Tanzania, Yassin Mohamed wa Polisi Tanzania.
Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar ni mshambuliaji.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA: NGUMU KUWAFUATILIA WACHEZAJI KWA SASA