Home Uncategorized MSHAMBULIAJI SIMBA AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUTUA YANGA

MSHAMBULIAJI SIMBA AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUTUA YANGA


 IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba, Charlse Ilanfya yupo kwenye hesabu za kutolewa kwa mkopo ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Sven Vandenbroeck huku timu yake ya zamani ya KMC ikitajwa kuwa miongoni mwa zile ambazo zinamhitaji pamoja na Yanga.

Ilanfya ambaye kabla ya kuibukia ndani ya Simba kwenye usajili wa dirisha kubwa msimu huu alikuwa kwenye hesabu za kutua Yanga msimu wa 2018/19 kabla ya dili lake kubuma na kuibukia ndani ya KMC na sasa yupo zake Simba.

Habari zinaeleza kuwa kutokana  na kuwekwa benchi ndani ya Simba kwa kuwa nafasi anayocheza ina washambuliaji tengemeo ambao ni John Bocco na Meddie Kagere amekuwa akiishia benchi.

Kwenye mechi 11 ambazo Simba imecheza ameanza kikosi cha kwanza mechi moja ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons jambo ambalo linamfungulia njia ya kuomba kutoka kwa mkopo.

 Ilanfya kuhusu jambo hilo amesema kuwa:”Bado sijapata taarifa rasmi na kuhusu kuomba kuondoka kwenda KMC ama Yanga hilo siwezi kulizingumzia kwa sasa,” .

Msimu uliopita akiwa ndani ya KMC alifunga mabao sita na kutoa pasi tatu za mabao jambo lililowafanya Simba kuisaka saini yake.

Kwa upande wa KMC, Christina Mwagala, Ofisa Habari wa timu hiyo amesema kwamba bado hawajapata taarifa kuhusu Ilanfya kutakiwa ndani ya kikosi hicho.

SOMA NA HII  WAWILI WAACHWA KMC MAZIMA