Home Uncategorized WAWILI WAACHWA KMC MAZIMA

WAWILI WAACHWA KMC MAZIMA


 WAKATI kipindi cha usajili wa dirisha dogo ukiendelea, KMC FC imeachana na wachezaji wake wawili.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala ambaye leo Januari Mosi ni kumbukizi yake ya kuletwa duniani ameseka kuwa nyota hao ni David Mwasa ambaye ameuzwa kwenda Mbeya City pamoja na Salim Aiyee kwa makubaliano ya pande zote mbili ya kusitisha mkataba wake.


Salimu alijiunga na KMC kwa mkataba wa miaka mwili akitokea Mwadui FC ambapo ameitumikia Timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi sita kabla ya mkataba wake kumalizika Juni 2021.

Kwa upande wa Mwasa ambaye alijiunga na KMC FC kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Lipuli, na hivyo kutumikia KMC FC kwa kipindi cha miezi sita kabla ya mkataba wake kumalizika Juni 2022.

KMC FC inawashukuru wachezaji hao kwa mchango mkubwa walioutoa wakati wa kitimiza majukumu yako na kwamba tunaimani kuwa watakwenda kufanya vizuri zaidi katika timu zao mpya watakazokwenda kuzitumia hivi sasa.


SOMA NA HII  YANGA YAIPIGA MKWARA AZAM FC, NYOTA WAO HUYU MMOJA KUKOSEKANA