Home Uncategorized NYOTA YANGA AMKARIBISHA MSHAMBULIAJI WA SIMBA KIKOSINI

NYOTA YANGA AMKARIBISHA MSHAMBULIAJI WA SIMBA KIKOSINI

MARCEL Kaheza mshambuliaji wa Polisi Tanzania anayekipiga kwa mkopo akitokea Klabu ya Simba amesema kuwa mshikaji wake Ditram Nchimbi anayekipiga ndani ya Yanga amemkaribisha kikosini humo.

Kaheza mkataba wake na Simba unameguka msimu huu utakapokamilika hivyo atakuwa mchezaji huru iwapo Simba hawatamuongezea dili jingine.

Pacha yake na Nchimbi ndani ya PolisiTanzania ilianza kujibu ambapo kwenye sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Yanga alimtengenezea pasi mbili za mabao Nchimbi ambaye alikuwa akicheza Polisi Tanzania na sasa yupo zake Yanga. “Nimekuwa nikiwasiliana na Nchimbi kwani sisi ni marafiki kwa muda mrefu, tulifanikiwa  kutengeneza pacha nzuri ndani ya Polisi Tanzania. “Nchimbi amekuwa akiniambia nipambane niwe bora muda wote ikiwezekana nipate dili la kuibukia Yanga ili tukiwashe tena pamoja,” amesema.

Kaheza ametupia mabao saba ndani ya Polisi  Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu,  Malale Hamsini.

SOMA NA HII  SENZO AMJIBU MOO DEWJI, ATAJA MKATABA WA LUIS MIQUISONE SIMBA SC