FAINALI ya Kombe la Shirikisho lililo mikononi mwa Azam FC mwaka huu itapigwa Sumbambawanga, mkoani Rukwa.
Uwanja huo wa Nelson Mandela kwa sasa unaendelea kufanyiwa maboresho ili fainali itakapofika uwe tayari kwa pambano hilo.
Mwaka 2019 fainali ya Kombe la FA ilipigwa Lindi na bingwa akawa Azam akishinda bao 1-0 mbele ya Lipuli likipachikwa na mshambuliaji Obrey Chirwa.
Kwa sasa mashindano ya Kombe la Shirikisho yapo hatua ya robo fainali ambapo tayari timu nane zimeshajua zitakutana na nani kwenye mechi zao.
Azam FC ambao ni mabingwa watetezi kete yao ni dhidi ya Simba, Kagera Sugar watakutana na Yanga, Ndanda FC itakuwa dhidi ya Sahare All Stars huku Namungo wao watakutana na Alliance FC.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.