Home Uncategorized AZAM FC SIO WATU WAZURI, WAIPIGA MABAO 2-0 MBAO FC

AZAM FC SIO WATU WAZURI, WAIPIGA MABAO 2-0 MBAO FC


AZAM FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo Uwanja wa Azam Complex.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Richard Djod dakika ya 49 kwa pasi ya Idd Naldo huku lile la pili likifungwa na Idd Chilunda dakika ya 90+3.

Ushindi huo unaifanya Mbao FC isalie nafasi ya 19 ikiwa na pointi zake 23 baada ya kucheza mechi 30.

Azam FC wao wanajiongezea ufalme nafasi ya pili wakiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 29.

SOMA NA HII  SAMATTA AUNGANA NA SERIKALI KUFANYA JAMBO LA KIHISTORIA