Home Uncategorized AZAM FC YAPANDISHA MAJEMBE SITA YA KAZI

AZAM FC YAPANDISHA MAJEMBE SITA YA KAZI


BENCHI la ufundi la Azam FC lililo chini ya Kocha Mkuu Aristica Cioaba limepandisha majembe sita ya kazi kutoka timu ya vijana ya umri wa miaka 20 (Azam U 20) na kufanya mazoezi kwenye kikosi cha wakubwa leo.

Azam FC inafanya mazoezi yake kwenye uwanja wao wa Azam Complex ambao nyasi zake zimefanyiwa maboresho hivi karibuni na kuingia kwenye anga za kimataifa zaidi.

Wachezaji hao sita ambao wamepandishwa leo na kufanya mazoezi na wakubwa ni pamoja na Emmanuel Kabelege, Shaban Kingazi, Omary Banda, Pascal Msindo, Samwel Onditi, Abdallah Madirisha.

SOMA NA HII  LALLANA AJIANDAA KUSEPA LIVERPOOL, ARSENAL, TOTTENHAM ZAPIGANA VIKUMBO