Home Uncategorized EYMAEL AUNGANA NA YANGA KAMBINI, KESHO KAZI KUANZA MBELE YA MWADUI FC

EYMAEL AUNGANA NA YANGA KAMBINI, KESHO KAZI KUANZA MBELE YA MWADUI FC



KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael leo amewasili kambini Shinyanga na kupokelewa na viongozi wa timu hiyo ambao walitangulia Juni 10.

Eymael alichelewa kujiunga na timu ambayo ilianza mazoezi tangu Mei 27 kwa kuwa alikuwa nchini Ubelgiji ambapo anga la ndege lilifungwa kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Yanga kesho itashuka uwanja wa Kambarage kumenyana na Klabu ya Mwadui FC kwenye mchezo wa ligi.

Eymael aliungana na wachezaji mazoezini ikiwa ni maandalizi ya mwisho kwenye mchezo huo wa kesho, Juni 13.

SOMA NA HII  JUMA KASEJA ASANI MIAKA KMC