Home Uncategorized HAWA HAPA WAKALI WA MIPIRA ILIYOKUFA NDANI YA YANGA NA AZAM FC

HAWA HAPA WAKALI WA MIPIRA ILIYOKUFA NDANI YA YANGA NA AZAM FC

KESHO Uwanja wa Taifa patachimbika kwa mechi kali kati ya Yanga dhidi ya Azam FC ambayo ni ya Ligi Kuu Bara.

Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 ambalo walijifunga wenyewe kupitia kwa beki wao Ally Mtoni,’Sonso’. 

Hawa hapa ni wakali wa kucheza na mipira iliyokufa ndani ya vikosi hivyo:-
Azam FC ina wakali watatu wa kutumia mipira iliyokufa.
Richard Djod ambaye kibindoni ana mabao manne alifunga bao moja kwa penalti.Agrey Morris ambaye ni nahodha ana bao moja ambalo alifunga kwa penalti pamoja na Nevere Tigere mwenye mabao matatu moja alifunga kwa faulo.
 Yanga wao mkali wao ni David Molinga ambaye amefunga mabao matatu kwa mipirailiyokufa. Amefunga kwa faulo mabao mawili na amefunga kwa penalti bao moja.
Patrick Sibomana ametupia bao moja alilofunga kwa mpira wa faulo ilikuwa mbele ya Ndanda FC kwa guu lake la kushoto.

Bernard Morrison ana bao moja alilowatungua Simba, Uwanja wa Taifa kwa faulo ndani ya ligi.
SOMA NA HII  RASMI...MSAUZI AMUONDOA TSHISHIMBI YANGA..!!