Home Uncategorized ISHU YA BAO LA SHEVA MBELE YA MBEYA CITY HAWA HAPA AMEACHIWA...

ISHU YA BAO LA SHEVA MBELE YA MBEYA CITY HAWA HAPA AMEACHIWA BAO LAKE


MIRAJ Atuman,’Sheva’ Kiungo mzawa mwenye uwezo mkubwa ndani ya Uwanja amesema kuwa bao lake alilowatungua Mbeya City anawaachia waamuzi kwa kuwa wao ndio wanajua kilichotokea.
Sheva Juni 24 Uwanja wa Sokoine wakati Simba ikishinda mabao 2-0 yote yakijazwa kimiana na nahodha John Bocco dakika ya 5 na 54, Sheva alifunga bao dakika ya 90+5 kwa pasi ya Clatous Chama,  lilifutwa na mwamuzi wa kati, Athuman Lazi kwa kile alichotafsiri kuwa mchezaji wa Mbeya City Keneth Kunambi alichezewa faulo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Sheva amesema kuwa hajui chochote kuhusu bao lake zaidi anamshukuru Mungu kwa kuwa timu yao imepata pointi tatu kibindoni.
“Goli langu mimi hata sijui inakuaje, hilo nawaachia waamuzi ila kikubwa ambacho ninafurahi kwa kuwa tumepata pointi tatu muhimu na maisha yanaendelea kwani kikubwa tunachohitaji ni pointi tatu hakuna kingine,” amesema Sheva.
Sheva kibindoni ana mabao sita na pasi moja ya mabao kati ya 69 ambayo yamefungwa na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 78 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 18 na pointi zake 30 zote zimecheza mechi 31.
SOMA NA HII  NYOTA WA SIMBA, BERNARD MORRISON NJE YA UWANJA MIEZI SITA