Home Uncategorized KOCHA MKUU WA YANGA ATIA TIMU BONGO

KOCHA MKUU WA YANGA ATIA TIMU BONGO

LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amewasili leo Dar es Salaam akitokea nchini Ubelgiji alikokuwa kwa ajili ya mapumziko ya lazima yaliyotokana na janga la Virusi vya Corona.

Eymael alichelewa kurejea Bongo baada ya Serikali kuruhusu masuala ya michezo kuanza Juni Mosi kutokana na anga ya Ubelgiji kufungwa ikiwa ni hatua ya kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Hakukuwa na mechi ya ushindani tangu Machi 17 mpaka pale Serikali iliporidhia kuruhusu masuala ya michezo kwa kueleza kuwa hali ya maambukizi imetulia.

Leo timu ya Yanga imeanza safari kuelekea Shinyanga ambapo kutakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa Juni 13 Uwanja wa Kambarage.

SOMA NA HII  NYOTA YANGA KASEKE AAHIDI MABAO 15