Home Uncategorized KUMBE SINGIDA UNITED WALIFANYA MAZOEZI SIKU TATU PEKEE KABLA YA KUWAVAA JKT...

KUMBE SINGIDA UNITED WALIFANYA MAZOEZI SIKU TATU PEKEE KABLA YA KUWAVAA JKT TANZANIA


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa ulifanya mazoezi kwa muda wa siku tatu kabla ya kuvaana na JKT Tanzania.

Singida United ilichapwa mabao 2-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kuifanya izidi kubaki kwenye nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 30.

Ramadhani Nswazurimo, Kocha Mkuu wa Singida United amesema kuwa walifanya mazoezi kwa muda wa siku tatu kabla ya kuingia uwanjani.

“Tulistahili kupoteza mbele ya JKT Tanzania kwa kuwa hatukufanya mazoezi kwa muda mrefu, baada ya Serikali kuruhusu masuala ya michezo tulifanya mazoezi siku tatu.

“Kwa sasa tunaendelea kujipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo kwani wachezaji wameanza kurejea kwenye ubora wao taratibu,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA IMESHAKUWA JANGA MO DEWJI AOGOPA KUFA KWA PRESHA