Home Uncategorized MWADUI FC YAPANIA KUBAKI KWENYE LIGI MSIMU UJAO

MWADUI FC YAPANIA KUBAKI KWENYE LIGI MSIMU UJAO


UONGOZI wa Mwadui FC umesema kuwa unajipanga kupata matokeo chanya kwenye mechi zake zilizobaki ndani ya Ligi Kuu Bara ili kubaki ndani ya ligi msimu ujao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Mwadui FC, David Chakala amesema kuwa wanakazi kubwa ya kutafuta matokeo kwenye mechi zao ili kujihakikishia nafasi ya kubaki kwenye ligi.

“Tuna mechi nyingi na ngumu ambazo zimebaki kwetu kwa sasa kwani ligi itakapoendelea kila timu itakuwa na hasira za kupata matokeo chanya.

“Wakati ule wa mapumziko ambayo yalisababishwa na Virusi vya Corona wachezaji walikuwa wakifanya mazoezi binafsi hivyo tuna imani hawatatuangusha,” amesema.

Juni 13 Mwadui FC iliyo nafasi ya 12 na pointi zake 34 baada ya kucheza mechi 28 itamenyana na Yanga mchezo wao wa kiporo ndani ya ligi.

SOMA NA HII  HAALAD: LAZIMA TUUNGANE KUPAMBANA NA CORONA, USIJIHISI UPO PEKE YAKO