Home Uncategorized NAMUNGO SASA KUKIWASHA MOTO NA YANGA TAIFA

NAMUNGO SASA KUKIWASHA MOTO NA YANGA TAIFA


NAMUNGO FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery Juni 24 itakuwa na kibarua cha kumenyana na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Machi 15, Uwanja wa Majaliwa, Namungo ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Yanga na kufanya wagawane pointi mojamoja.

Mchezo wake uliopita, Juni 20 Namungo ilishinda mabao 2-0 Uwanja wa Majaliwa mbele ya Kagera Sugar.

Yanga mchezo wake uliopita, Juni 21 ililazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC Uwanja wa Taifa.

Luc Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anahitaji kuona vijana wake wakipata pointi tatu huku Thiery wa Namungo akisema kuwa wapo tayari kwa ushindani. 

SOMA NA HII  MAGURI UNGANA NA KESSY ZAMBIA