Home Uncategorized POLISI TANZANIA BADO HAIJAREJEA KWENYE UBORA WAKE

POLISI TANZANIA BADO HAIJAREJEA KWENYE UBORA WAKE


MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa kikosi chake bado hakijarejea kwenye ubora wake kutokana na kutokuwa na muunganiko mzuri baada ya kurejea uwanjani.

Masuala ya michezo yalisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Corona ila kwa sasa Serikali imeridhia masuala ya michezo kuendelea kwa kueleza kuwa hali ya maambukizi imepungua.

Kwenye mchezo uliochezwa Juni 20, Polisi Tanzania ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Lipuli mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Ushirika Moshi.

Malale amesema:”Bado ule muunganiko wa kikosi haujaanza kurejea huu ndio ukweli wenyewe ila bado tunajipanga kuona namna gani ile kasi yetu itarejea.”

Bao la Polisi Tanzania lilifungwa na kiungo Baraka Majogoro huku lile la kusawazisha kwa Lipuli likifungwa na Rashid Hassan.

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING: WAO WANA PIRA BIRIANI SISI TUNA PIRA KAVUKAVU