Home Uncategorized HAPA NDIPO LILIPO TATIZO LA MBEYA CITY

HAPA NDIPO LILIPO TATIZO LA MBEYA CITY


AMRI Said, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa mfumo wake wa kucheza mipira mirefu ni tatizo jambo ambalo analifanyia kazi kwenye mechi zake zinazofuata.

Juni 20, Mbeya City ilikubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Alliance kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine.

Ana kibarua kingine tena Juni 24 Uwanja wa Sokoine kumenyana na Simba ambayo tayari imeshatia timu ndani ya jiji la Mbeya.

 Said amesema:”Wachezaji wangu walikuwa na kazi kubwa kwenye mchezo wetu dhidi ya Alliance kuendana sawa na mfumo ule wa mipira mirefu jambo ambalo liliwapa shinda hasa kwa namna ya kuzuia mashambulizi ila kwa kuwa mchezo wetu umeshapita tunajipanga kwa ajili ya mechi zinazofuata.”

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa, Mbeya City ilalala kwa kuchapwa mabao 4-0 wakati ule ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Juma Mwambusi.

SOMA NA HII  NGOME MPYA YATENGENEZWA SIMBA