Home Uncategorized NYOTA SABA WA AZAM FC WAMPA WAKATI MGUMU CIOABA

NYOTA SABA WA AZAM FC WAMPA WAKATI MGUMU CIOABA


KOCHA Mkuu wa Azam FC, Mromania Aristica Cioaba amekiri kuwa anapata wakati mgumu wa kukiandaa kikosi kurejea kwenye michezo ya ligi kuu bila uwepo wa wachezaji wake saba wakimataifa.

Cioba amesema kuwa wachezaji wote saba ambao wamekwama kwenye nchi zao kutokana na ‘Lockdown’ wanacheza katika nafasi muhimu kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, hivyo kuwakosa ni pengo kubwa sana kwa timu yake.

Wachezaji wa Azam ambao bado hawajajiunga na timu hiyo ni mabeki wa kati wawili raia wa Ghana, Yakubu Mohammed, Daniel Amoah na golikipa namba moja wa timu hiyo Razack Abarola. Wengine ni Bruce Kangwa, Never Tigere na  Donald Ngoma wote ni Wazimbabwe na Nickolas Wadada raia wa Uganda.

 Cioaba amesema itakuwa ngumu wao kuiwahi michezo ya kwanza kwa kuwa nchi zote ambazo wachezaji hao wanatoka bado zipo kwenye ‘Lockdown’ na kufunguka kuwa jambo alilofanya kwa sasa ni kuwapandisha wachezaji kutoka timu B na kuanza kujenga kikosi mbadala.

“Sina uhakika kama wachezaji hao watakuwa sehemu ya kikosi katika michezo ya kwanza ya ligi kuu kwa sababu nchi zao zipo kwenye ‘Lockdown’, naumiza kichwa kuona nitafanyaje kwa sababu nimejaribu pia kuwapandisha wachezaji kutoka timu B, lakini bado wanahitaji zaidi ya wiki mbili kuingia kwenye mfumo,” amesema Cioaba.

Chanzo:Championi
SOMA NA HII  KMC YAWEKA KANDO KICHAPO CHA MTIBWA SUGAR, HESABU ZAO KWA MABINGWA WATETEZI