Home Uncategorized SHIKHALO AFUNGUKIA ISHU YA KUWEKWA BENCHI NA MNATA

SHIKHALO AFUNGUKIA ISHU YA KUWEKWA BENCHI NA MNATA


FAROUK Shikhalo, mlinda mlango namba moja wa Yanga amesema kuwa kukaa kwake benchi kwenye mechi za Ligi Kuu Bara kunampa hasira ya kujinoa zaidi ili awe fiti wakati mwingine.
Nyota huyo ambaye ni raia wa Kenya aliwekwa benchi na kipa namba mbili wa Yanga, Metacha Mnata kwenye mechi tatu walizocheza Yanga, Shinyanga, Juni 13 mbele ya Mwadui FC, Dodoma, mbele ya JKT Tanzania Juni 17 na mbele ya Azam FC, Juni 21.
Akizungumza na Saleh Jembe, Shikhalo amesema kuwa kila mchezaji ndani ya Yanga ni lazima acheze kulingana na mahitaji ya mwalimu jambo ambalo halimpi presha.
“Kila mchezo una falsafa zake na mwalimu anajua ni nani anastahili kuanza kwenye mechi husika, kukaa kwangu benchi haina maana kwamba siwezi hapana ni maamuzi ya mwalimu na kwa hali hiyo inanifanya nizidi kupambana ili kuwa bora,” alisema Shikhalo
SOMA NA HII  NYOTA AZAM FC ACHEKELEA MAISHA YAKE KWA SASA, APANIA MAKUBWA