Home Uncategorized UNAKUMBUKA ZILE HABARI ZA SHONGA KUTUA SIMBA??… SASA MAMBO YAPO HIVI..!!!

UNAKUMBUKA ZILE HABARI ZA SHONGA KUTUA SIMBA??… SASA MAMBO YAPO HIVI..!!!

INAELEZWA mshambuliaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Mzambia Justin Shonga yupo mbioni kujiunga na Klabu ya CS Maritimo ya nchini Ureno, hiyo ni baada ya kushindwana na Simba.

 Shonga inaonekana ameshindwana na klabu hiyo kwa kuwa dau lake la usajili lipo juu sana.Mshambuliaji huyo raia wa Zambia mwenye uwezo mkubwa wa kufunga, thamani yake sokoni ni euro 600,000 (zaidi ya Sh bilioni moja), sasa huenda hiyo ilikuwa kikwazo kikubwa kwa Simba ambayo ilikuwa imeshakubali kumlipa mshahara wa Sh mil 34 kwa mwezi, kwa mujibu wa watu wake wa karibu.

 Taarifa za uhakika kutoka kwa mtu wa karibu wa mshambuliaji huyo anayeishi Afrika Kusini, zinasema kuwa mshambuliaji huyo anajipanga kuelekea barani Ulaya baada ya kupata timu hiyo kutokana na kugomea ofa za klabu za Afrika alizokuwa akipokea.

 Chanzo hicho kilisema kuwa Mzambia huyo anatarajia kutimkia kwenye nchi hiyo baada ya mazungumzo yake na klabu ya CS Maritimo ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Ureno kuwa katika hali nzuri.

“Shonga amefanya maamuzi ya kubadilisha upepo kwa sababu ameamua kwenda kucheza Ulaya na atakwenda nchini Ureno kujiunga na klabu ya CS Maritimo kwa sababu timu nyingi za Afrika zimeshindwa kufi kia muafaka naye.

 “Sasa hivi kumekuwa na mazungumzo na Orlando kwa kuwa bado wao ndio wanammiliki kwa sababu ya mkataba wake lakini kwa upande wa mchezaji ameonyesha utayari kwa kwenda kucheza Ureno na siyo kuendelea kucheza Afrika,” kilisema chanzo.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA AIBUKA TENA NA TAMKO LA AINA YAKE, AONESHA KUSHANGAZWA