Home Uncategorized WACHEZAJI WA CHELSEA KUWEKEWA MSOSI KWENYE GARI

WACHEZAJI WA CHELSEA KUWEKEWA MSOSI KWENYE GARI


KLABU ya Chelsea imepanga kuwapelekea chakula wachezaji wake ndani ya gari baada ya mazoezi ili kujenga miili yao kutokana na sheria ya kuzuia mijumuiko isiyo ya lazima kuendelea.

Sheria hiyo ina lengo la kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vilisababisha kusimamishwa kwa shughuli nyingi duniani ikiwa ni pamoja na michezo.

Kwa sasa matumizi ya kanteen kwa wachezaji pamoja na wafanyakazi yamekatazwa jambo ambalo limewafanya viongozi kufikiria mbinu mbadala ya kuwapa chakula wachezaji wao wanaojiandaa na kurejea kwa Ligi Kuu England Juni 17.

Imeripotiwa kuwa wakati Kocha Mkuu, Frank Lampard akiwa anakinoa kikosi chake wapishi watakuwa jikoni wakipika na kuweka msosi ndani ya gari la kila mchezaji ambao ataufinya na mwingine kwenda nao nyumbani.

SOMA NA HII  YANGA:TUMEANDAA SARE KWA AJILI YA SIMBA