Home Uncategorized YANGA YASITISHA MKATABA WA KATIBU RUHANGO

YANGA YASITISHA MKATABA WA KATIBU RUHANGO


 KLABU ya Yanga imefika makubaliano ya kusitisha ajira ya  Dr.David Luhago aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo.

Taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa Yanga imeeleza kuwa wamekubaliana kusitisha nafasi yake ya kazi kuanzia leo Juni 15.

Kamati ya Utendaji ya Yanga iliyo chini ya Mwenyekiti wa Klabu hiyo Dr, Mshindo Msolla imemshukuru kiongozi huyo kwa ushirikiano wake.

SOMA NA HII  MRITHI WA NDAYIRAGIJE NDANI YA KMC HUYU HAPA