DAVID Molinga mtupiaji namba moja ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa wamekubaliana kwa pamoja kupata pointi tatu kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Biashara United.
Molinga mwenye mabao 10 ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ni kinara wa utupiaji ndani ya klabu hiyo iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael ambayo imefunga jumla ya mabao 38 baada ya kucheza mechi 32.
Leo Yanga itakaribishwa na Biashara United inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza ambaye alitoka kulazimisha sare mbele ya Azam FC kwa kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Karume.
Molinga amesema:”Wachezaji tupo tayari na kila mmoja anajua kwamba tunahitaji pointi tatu, nafasi ambayo tupo kwa sasa ina ushindani mkubwa hivyo ili kuzidi kubaki kwenye nafasi tuliyopo ni lazima tushinde.”
Mpinzani mkubwa wa Yanga kwa sasa kwenye nafasi ya pili ni Azam FC mwenye pointi 59 baada ya kucheza mechi 59 ishu ya ubingwa ipo mikononi mwa Simba.