Home Uncategorized BREAKING:MECHI ZA LIGI KUU BARA KUPANGIWA TAREHE

BREAKING:MECHI ZA LIGI KUU BARA KUPANGIWA TAREHE


KUTOKANA na kifo cha Rais wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, kilichotokea usiku wa kuamkia leo, kuna uwezekano mkubwa wa mechi za Ligi Kuu Bara kupangiwa tarehe.

Julai 26 ligi ilitarajiwa kumalizika kwa timu 20 kuingia uwanjani kusaka pointi tatu muhimu na kuweza kutambua hatma ya timu ambazo zitashuka daraja na kucheza playoff.

Kutokana na Julai 26 mpaka Julai 28 kutangazwa na Serikali kuwa ni siku ya kuaga mwili wa Mkapa na 29 Julai atapumzishwa Mtwara Bodi ya Ligi Tanzania imesema kuwa kuna uwezekano wa kupanga tarehe upya za mechi za Julai 26.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Tanzania, Steven Mguto alisema:”Ni msiba mkubwa kwa Taifa na ukizingatia kwamba Julai 26 anaagwa ni lazima tupange siku nyingine ya mechi kuchezwa ila kwa sasa ngoja tuangalie kwanza na bodi kwa pamoja kisha tutatoa taarifa.”

SOMA NA HII  MARIO GOTZE ASAINI DILI LA MIAKA MIWILI PSV