Home Uncategorized CHAMA CLATOUS AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUIBUKIA YANGA

CHAMA CLATOUS AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUIBUKIA YANGA


CLATOUS Chama, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa hana hiyana iwapo atahitajika kukipiga ndani ya Yanga kwani kazi ya mchezaji ni kucheza mpira.

Chama amekuwa kwenye ubora wake msimu huu wa 2019/20 kwa upande wa kutengeneza pasi za mwisho ambapo anazo jumla 11 na amefunga mabao sita.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa Yanga inahitaji kupata saini ya nyota huyo ikiwa na lengo la kuboresha kikosi chao kwa msimu ujao.

Chama amesema:” Kwa mchezaji kazi yake ni kucheza bila kujali yupo wapi ila kikubwa ni utaratibu kufuatwa kwani kwa sasa nipo ndani ya Simba.

“Bado nina mkataba na Simba kwa timu ambayo itakuwa inahitaji saini yangu ni lazima iwasiliane na uongozi wa Simba,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA YAZIDI KUFANYA KUFURU, MCHEZAJI MWINGINE MPYA ASAINI MIAKA MITATU - VIDEO