Home Uncategorized FT: COASTAL UNION 0-0 SIMBA, WAWA AONYESHWA KADI NYEKUNDU

FT: COASTAL UNION 0-0 SIMBA, WAWA AONYESHWA KADI NYEKUNDU


MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Coastal Union na Simba uliochezwa leo, Julai 23 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga umekamilika kwa timu zote kutoshana nguvu bila kufungana ndani ya dakika 90.

Coastal Union inayonolewa na Juma Mgunda ililiandama lango la Simba kipindi cha pili kwa kumtumia mtupiaji wao namba moja Ayoub Lyanga mwenye mabao nane ndani ya ligi ila mikono ya Beno Kakolanya iliokoa hatari zake.

Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck ilikuwa ikifanya mashambulizi kwa kumtumia Meddie Kagere na John Bocco mambo yalikuwa magumu kwao.

Bocco alitolewa kipindi cha pili nafasi yake ikachukuliwa na Clatous Chama na Miraj Athuman alitolewa ia nafasi yake ikachukuliwa na Deo Kanda ila ngome ya Coastal Union chini ya Bakari Nondo ilibaki kuwa imara.

Pascal Wawa alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa leo baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano hivyo Simba ilimaliza dakika tisini ikiwa na wachezaji 10 baada ya beki huyo wa kigeni kutolewa dakika ya 75.

Atakuwa akiwashuhudia wenzake kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Polisi Tanzania, Ushirika, Moshi.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 85 baada ya kucheza mechi 37, Coastal Union inafikisha jumla ya pointi 53 zote zinauhakika wa kubaki ndani ya ligi.

SOMA NA HII  NYOTA YANGA AMKOSESHA AMANI KIPA TOWNSHIP ROLLERS