Home Uncategorized HUYU HAPA MRITHI WA MIKOBA YA EYMAEL YANGA

HUYU HAPA MRITHI WA MIKOBA YA EYMAEL YANGA


INAELEZWA kuwa kocha wa zamani wa Yanga Hans Pluijm anakuja kubeba mikoba ya Mbelgiji Luc Eymael ndani ya Yanga.

Eymael amefukuzwa kazi ndani ya Yanga kutokana na vitendo vyake vya kibaguzi jambo ambalo limepelekea uongozi wa Yanga kuamua kuachana naye.

Julai 26 baada ya kumaliza ligi kwa kuishusha Lipuli FC ya Iringa Uwanja wa Samora kwa ushindi wa bao 1-0 ilisambaa sauti yake akisema kuwa hafurahishwi na mambo yanayofanyika ndani ya Tanzania pamoja na mashabiki kutokujua masuala ya soka.

Habari zinaeleza kuwa tayari Yanga wamefanya mawasiliano na Pluijm ili kurejea tena ndani ya Bongo kukinoa kikosi hicho.

“Tayari kwa sasa uongozi umeanza kufanya mawasiliano na Hans, mambo yakiwa sawa anaweza kutua ndani ya Bongo kukinoa kikosi cha Yanga,” ilieleza taarifa hiyo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga,Simon Patrick amesema kuwa masuala ya benchi la ufundi yanashughulikiwa kwani ni mapema kwa sasa shughuli ya kwanza ni kuondoka kwa Eymael.  

SOMA NA HII  FUNDI WA KUCHEKA NA NYAVU ATOA TAMBO ZA KUTOSHA KABLA YA KUTUA YANGA