Home Uncategorized SIMBA YAJICHIMBIA KWA SASA MBEYA WAKIIVUTIA KASI NAMUNGO

SIMBA YAJICHIMBIA KWA SASA MBEYA WAKIIVUTIA KASI NAMUNGO


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa wachezaji wote wapo salama wakiwa tayari kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa Agosti 2.

Fainali hiyo itapigwa Uwaja wa Nelson Mandela, Sumbawanga inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Akizungumza na Saleh Jembe, meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wapo Mbeya kwa sasa kabla ya kuelekea Sumbawanga kwa ajili ya mchezo huo.

“Kikosi kwa sasa kipo salama na muda huu tupo Mbeya kabla ya kuelekea Sumbawanga, kwani bado kuna siku kadhaa hapa mpaka itakapofika Agosti 2, 2020.

“Wachezaji wana morali kubwa na kila kitu kipo sawa kuelekea kwenye fainali hivyo sisi tupo tayari,” amesema.

Simba ilitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Yanga huku Namungo ikishinda bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars.

SOMA NA HII  SportPesa YAMKABIDHI MSHINDI WA JACKPOT SportPesa MAMILIONI