Home Uncategorized HUYU NDIYE STAA WA SIMBA ALIYEWAVURUGAVURUGA YANGA, WALICHOMFANYA UWANJANI NAYE ALIWALIPA HAPOHAPO

HUYU NDIYE STAA WA SIMBA ALIYEWAVURUGAVURUGA YANGA, WALICHOMFANYA UWANJANI NAYE ALIWALIPA HAPOHAPO


KIUNGO wa Simba, Luis Miqussone, raia wa Msumbuji, ameonekana kuwa moto wa kuotea mbali, labda kuliko staa mwingine kwenye timu hiyo kwa sasa.
Huyu ndiye alikuwa staa kwenye mchezo wa nusu fainali wa Kombe la FA kati ya Yanga na Simba ambao Simba walishinda kwa mabao 4-1.

Kiungo huyo ambaye alifunga bao moja kwenye mechi hiyo, ndiye mchezaji aliyeonekana kuwa bora zaidi kwenye mechi hiyo iliyopigwa Julai 12 Uwanja wa Taifa.
Luis anaweza kuwa mchezaji mgeni mwenye uwezo wa juu sasa hapa nchini akiwa amefanya mambo ya ajabu kwenye dakika tisini za mchezo huo.Staa huyo alichezewa rafu mara nne ambazo mwamuzi aliziona akiwa ndiye alichezewa rafu nyingi zaidi.
Alifanikiwa kupiga jumla ya pasi 23, huku tatu zikiharibika kwa dakika zote tisini, lakini akifunga bao moja, alipiga mashuti matatu moja likizaa bao na ndani ya boksi alipiga kichwa mara moja kilichopaa juu.Katika mchezo huo alionekana kuwa hatari zaidi baada ya kuingia kwenye boksi mara tisa zaidi ya mchezaji mwingine katika mchezo huo.
Hata bao lake alilofunga alitoka mwenyewe na mpira nyuma na kwenda kutengeneza pasi ambayo alirudishiwa tena na kufunga. Huyu unaweza kumwita mashine kwenye mchezo huo na ni ngumu kwa Yanga kusahau kile ambacho alikifanya kwenye mechi hiyo.
Staa huyo raia wa Msumbiji alisema kuwa amefurahishwa kuwa mmoja ya wafungaji katika mchezo huo uliowapeleka kucheza fainali ya kombe hilo.
“Kitu kikubwa nilifanya kwenye dabi ni kuweza kufunga moja kati ya mabao muhimu kwenye timu yangu kwa sababu tulijiandaa kupata ushindi ambao tumestahili.
“Nadhani hili limeshapita kwa upande wetu lazima tuangalie yaliyo mbele yetu hasa ubingwa wa Kombe la FA, katika mchezo ujao wa fainali kwamba nini tutaweza kufanya lakini kuhusu tena Yanga ambao tumewafunga mabao mengi, imekuwa furaha kwetu,” alisema Luis.
SOMA NA HII  CHEKI MOTO WA KIKOSI BORA CHA MSIMU WA 2019/20