Home Uncategorized KUMEKUCHA YANGA, MAJEMBE HAYA MANNE YA KAZI KUSEPA MAZIMA

KUMEKUCHA YANGA, MAJEMBE HAYA MANNE YA KAZI KUSEPA MAZIMA


INAELEZWA kuwa nyota wanne ndani ya Yanga msimu ujao hawatakuwa ndani ya kikosi hicho kutokana na sababu mbalimbali ambazo zimetajwa ikiwa ni pamoja na ile ya kuboresha kikosi kazi.

Yanga inapambana kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili kwa sasa inanolewa na Kocha Mkuu, Luc Eymal raia wa Ubelgiji ambaye ametoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mwadui FC, Uwanja wa Taifa.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa kuondoka ndani ya Yanga msimu wa 2020/21 ni pamoja na mtupiaji namba moja ndani ya Yanga, David Molinga mwenye mabao 10 na pasi moja ya bao.

 Molinga inadaiwa ameshapata timu nyingine ya kujiunga nayo nje ya Tanzania.

Mkongwe ndani ya kikosi hicho, Mrisho Ngassa fundi wa mpira yeye inaelezwa kuwa amepata ofa nchini Kenya na dili lake ndani ya Yanga linakaribia kuisha.

 Andrew Vicent ‘Dante’ na Tariq Seif mwenye mabao matatu, wanatajwa kutokuwa kwenye mpango wa Eymael.

SOMA NA HII  MANARA : - SIMJUI YOYOTE NCHI HII...HAKUNA WAKUNISOGELEA...SIPOI HATA TONE LABDA WAJE KUNIUA....