Home Uncategorized LUIS ATEMBEZA BONGE MOJA YA MKWARA KWA MABEKI

LUIS ATEMBEZA BONGE MOJA YA MKWARA KWA MABEKI


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone, raia wa Msumbiji, ni kama amewatangazia kiama mabeki wa ligi kuu kwa kuwaambia licha ya kwamba wanamfanyia faulo nyingi lakini hawezi kuwaogopa.

Luis amesema kwamba licha ya kufanyiwa rafu nyingi uwanjani na mabeki kama njia ya kumzuia lakini kwake ataendelea kuwapiga chenga kwa sababu ndiyo kazi yake inayomfanya awepo uwanjani.

Kiungo huyo amesema kuwa licha ya kwamba anakutana na faulo nyingi, ataendelea kusukuma mashambulizi.

“Hii ni kazi yangu kuhakikisha nasukuma mashambulizi kwa wapinzani wetu, hata wakinifanyia faulo bado natakiwa kuwafuata na kupambana nao.

“Siogopi majeraha kwa sababu ya muda mwingine kuhitajika kusukuma mashambulizi kwa mabeki wa timu pinzani, hivyo hata kama hilo linatokea lakini sitakiwi kurudi nyuma,” alisema Luis.

Staa huyo aliyetua Simba akitokea UD do Songo ya Msumbiji alipokuwa akicheza kwa mkopo, hadi sasa amefunga mabao matano tangu aingie kikosini hapo. Manne kwenye ligi, moja la Kombe la Shirikisho.
SOMA NA HII  KOCHA MANCHESTER CITY AWAPA SOMO MASHABIKI NA WACHEZAJI KUHUSU CORONA