Home Uncategorized MBAO FC KUPAMBANIA NAFASI YA KUBAKI NDANI YA LIGI KESHO MBELE YA...

MBAO FC KUPAMBANIA NAFASI YA KUBAKI NDANI YA LIGI KESHO MBELE YA NAMUNGO


KOCHA Mkuu wa Mbao FC, Felix Minziro amesema kuwa atapambana mbele ya Namungo FC kwene mchezo wa kesho Julai 22, utakaochezwa Uwanja CCM Kirumba.

Mbao FC ipo kwenye hatari ya kushuka daraja ikiwa itashindwa kushinda mechi zake mbili zilizobaki kwa sasa haina uhakika wa kubaki iwapo wale walio juu yake watashinda mechi zao.

Ipo nafasi ya 19 ikiwa imecheza jumla ya mechi 36 kibindoni ina pointi 39.

“Tumetoka kugawana pointi na JKT Tanzania hii inazidi kutuweka kwenye hatari zaidi na sare hiyo ilitokana na uchovu wa wachezaji kwani tulikuwa na safari ndefu lakini hatujakata tamaa.

“Mechi yetu dhidi ya Namungo licha ya kwamba tutakuwa nyumbani itakuwa ni ngumu kwani tunacheza na timu ambayo ina kasi na ina wachezaji wengi wenye uwezo ndani ya uwanja.

“Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti ili kuona namna gani tutatoa burudani na kusaka pointi tatu muhimu,” amesema.

Ikimalizana na Namungo FC ina kibarua kingine cha mwisho mbele ya Ndanda FC ambao nao pia wanapambana kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja.

Ndanda ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 40 baada ya kucheza mechi 36.

SOMA NA HII  BEKI MTIBWA SUGAR MIKONONI MWA KAZE