Home Uncategorized BEKI MTIBWA SUGAR MIKONONI MWA KAZE

BEKI MTIBWA SUGAR MIKONONI MWA KAZE

 


IMEELEZWA kuwa beki wa Klabu ya Mtibwa Sugar,  Hassan Kessy amewekwa kwenye rada za mabosi wa kikosi hicho ili kumrejesha kundini.


Kessy alikuwa kwenye hesabu za kujiunga na Yanga msimu huu baada ya kumaliza mkataba wake na Klabu ya Nkana FC ila mambo yalibuma kutokana na ishu ya dau kuwa kubwa.

Kwa sasa yupo zake Mtibwa Sugar akiendelea kusaka ugali wa kila siku kupitia kazi yake hiyo anayoipenda kwa wakati huu.

Habari zimeeleza kuwa Kocha Mkuu Cedric Kaze anamtazama beki huyo ili aweze kumuunganisha ndani ya kikosi hicho kwenye usajili wa dirisha dogo ambalo limefunguliwa Desemba 16.

“Kaze amepewa jukumu la kufanya usajili kwa wachezaji ambao anahitaji na kwa namna kikosi kilivyo nadhani hakutakuwa na usajili wa kutisha zaidi ya kuboresha kidogo tu.

“Miongoni mwa nyota ambao anawafuatilia ni pamoja na Kessy,(Hassan) hivyo akikubali uwezo wake anaweza kurudishwa kundini,” ilieleza taarifa hiyo.

Kaze kuhusu usajili amesema:”Kwa sasa ngoja nimalize hizi mechi ambazo zipo mbele yangu nikitulia nitazungumza na uongozi nini kinahitajika,”.
SOMA NA HII  AZAM FC: KICHAPO CHETU MBELE YA NAMUNGO HATUNA WA KUMLAUMU