Home Uncategorized YANGA NA SIMBA WAINGIA VITANI KUSAKA SAINI YA BEKI HUYU MZAWA

YANGA NA SIMBA WAINGIA VITANI KUSAKA SAINI YA BEKI HUYU MZAWA


EDWARD Manyama, beki wa kushoto wa Klabu ya Namungo inaelezwa kuwa amewekwa Kwenye rada za Simba na Yanga.

Yanga walianza kumvutia kasi mzawa huyo ambaye aliwahi kucheza pia kwenye kikosi hicho ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho ambacho kinawania ubingwa.


Kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze kinaongoza Ligi Kuu Bara na kibindoni kina pointi 40 na kimecheza jumla ya mechi 16.

 Beki huyo wa kushoto ni mtaalamu pia wa kupiga mipira iliyokufa ambapo walipokutana na Azam FC, Uwanja wa Azam Complex alimtungua kipa namba mbili Benedict Haule kwa faulo aliyoipiga akiwa nje kidogo ya 18.


Habari zinaeleza kuwa Simba nao wapo kwenye hesabu za kuwania saini ya beki huyo ili akamuongezee changamoto Hussein Mohamed ambaye kwa sasa anapambana na Gadiel Michael.


Kuhusu usajili ndani ya Yanga, Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo amesema kuwa jukumu lote lipo mikononi mwa kocha ambaye anajua anahitaji aina gani ya wachezaji.

SOMA NA HII  MECHI YA AZAM VS GOR MAHIA YAPEPERUKA ISHU IKO HIVI